Tetesi za Usajili nchini Tanzania kwa klabu za Ligi Kuu

Wakati Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) likiwa limefunguliwa Agosti 1,2020. Huku Klabu zikitarajiwa kufanya usajili kwa muda wa mwezi mmoja ambapo dirisha litafungwa Agosti 31 saa 5:59 usiku, hizi ndiyo tetesi za Usajili kwa sasa Tanzania.

Zawadi Peter Mauya @giftmauya ametia saini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia Wananchi kabu ya Yanga. (Yanga)

Beki kisiki, Bakari Nondo Mwamnyeto @bakarmwamnyeto amejiunga na kikosi cha Timu ya Wananchi, Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili. (Yanga)

Timu ya Wananchi imeendelea kujiimarisha baada ya kuinasa saini ya Yassin Mustapha Salum @yassaboy23 kutoka Polisi Tanzania.(Yanga)

Harakati zinaendelea kuimarisha kikosi cha Timu ya Wananchi na jana wamemalizana na mshambuliaji mahiri, Waziri Junior @wazir_junior_10 kutoka Mbao FC. (Yanga)

Inadaiwa Simba SC inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ghana, Michael Sarpong baada ya kufeli kwa mazungumzo baina ya Mghana huyo na klabu ya Rayon Sports

Mabingwa wa nchi Simba SC wamehusishwa na kutaka kumsajili mshambulia raia wa Zambia, Justine Shonga ambaye anakipiga nchini Afrika Kusini kunako klabu ya Orlando Pirates.

Kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari kutoka Zambia vinadai Simba inavutiwa na nyota huyo na ghara za Shonga ni dola za Kimarekani 550,000.

Simba imehusishwa katika kumhitaji beki wa Harambee Stars, Michael Kibwage licha ya taarifa hizo kukataliwa na mchezaji mwenyewe. Beki huyo wa KCB ameonekana kufanya vizuri.

Harambee Stars defender denies Simba SC links

 

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Ismail Aziz Kada, amefuzu vipimo vya afya, tayari kabisa kujiunga na timu kizazi kipya ya Azam FC kwa ajili ya msimu ujao. (Azamfc)

Kiungo mshambuliaji, Ayoub Lyanga, amekamilisha taratibu za kujiunga na Azam FC, baada ya kusaini mkataba rasmi wa miaka miwili akitokea Coastal Union, kwa usajili huru.

Nyota huyo amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu akiisaidia vilivyo Coastal, akifunga jumla ya mabao nane (4) kwenye ligi na kuchangia pasi nane zilizozaa mabao. (Azam fc)

Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima, kwa mkataba wa miaka miwili.

Niyonzima aliyekuwa akicheza Rayon Sports ya Rwanda, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba. Amesaini mkataba Jumamosi mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’. (Azamfc)

Azam FC wamekamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu, kwa mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo ambaye aliwahi kulelewa kwenye kituo cha Azam Academy kwa miaka miwili 2014-2015, amesaini mkataba huo Alhamisi jioni mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’. (Azamfc)


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais