Aston Villa kumng’oa mshambuliaji wa Liverpool
Kocha wa Aston Villa, Dean Smith anakusudia kukiimarisha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji baada ya kufanikiwa kuepuka kushuka dara kutoka Premier League.
Katika kuhakikisha inafanikiwa katika hilo, wamekusudia kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Ubelgiji Divock Origi, 25.
Origi amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 44 pekee ndani ya Liverpool msimu huu uliyomalizika, lakini mara zote amekuwa mtu wa kusugua benchi akiwapisha Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wakianza.(Sun)
Mabingwa wa kombe la FA klabu ya Arsenal wanamlia rada beki wa kati raia wa Brazil, Diego Carlos huku Mikel Arteta akikusudia kukisuka upya kikosi chake kwaajili ya msimu ujao. (Telegraph – subscription required)
Arsenal inatarajia kutoa ofa nono kwa mshambuliaji wake raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang 31, wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo. (Mirror)
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda. (Mail)
Liverpool imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania. (Mundo Deportivo, via talkSPORT)
Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil, 22. (RMC Sport, via Express)
Wakati huohuo, United inamatumaini ya kumtumia mlinzi Chris Smalling, 30, katika makubaliano ya mabadilishano na mlinzi wa Inter Milan, 25, raia wa Slovakia Milan Skriniar – lakini Roma inaendelea na machakato wake wa kumtafuta Mwingereza baada ya kuiridhisha timu hiyo alipokuwa kwa mkopo. (Star)
Mabingwa wa Italia AC Milan na Napoli inafanya mazungumzo na mlinzi wa Uingereza wa timu ya Norwich City, Ben Godfrey, 22, baada ya Canaries kushushwa daraja kwenye ligi ya Premier. (Calciomercato, via Mail)
Cardiff City inaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka, 27, wa Barnsley na mshambuliaji wa Wales Kieffer Moore. (WalesOnline)
Comments