Maximo Rasmi Atuma CV Zake Yanga


JINA la Mbrazili, Marcio Maximo ni kati ya makocha 60 waliotuma maombi ya kuifundisha Yanga katika msimu ujao.

Yanga ipo kwenye mchakato wa kumpata kocha mpya atakayekuja kuinoa timu hiyo baada aliyekuwa kocha Mbelgiji, Luc Eymael kutimuliwa. Kocha mwingine anayetajwa kuwania kibarua cha Mbelgiji huyo ni Mfaransa, Patrick Aussems.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Championi Jumatatu, Maximo amewasilisha maombi ya kuja kuifundisha timu hiyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kocha huyo ametuma CV zake wiki iliyopita na kuungana na makocha wengine 59 walioomba kukinoa kikosi hicho.

Aliongeza kuwa uongozi wa timu hiyo umepanga kukutana wiki hii kwa ajili ya kupitia maombi na CV za makocha wote kabla ya kufanya mchujo. Maximo hivi karibuni aliliambia gazeti hili kuwa:

“Nipo tayari kujiunga na Yanga kama wakinihitaji, hivi sasa nipo nafundisha timu ya taifa ya Naguya iliyopo Amerika Kusini.”


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele