Ndinga la bei mbaya lamponza mchezaji wa Premier League mwenye asili ya Afrika
Beki wa Tottenham mwenye asili ya Afrika, Danny Rose amesimulia namna alivyojikuta akisimamishwa na Polisi huku akikutana na maswali lukuki kutokana na gari la bei mbaya alilokuwa akiendesha wakati akirudi nyumbani kwake.
Danny Rose mwenye umri wa miaka 30, amesimulia namna alivyosimamishwa na Polisi ghafla wakati akirudi nyumbani kwake Doncaster tukio lililotokea wiki iliyopita.
Rose amesema mara kadhaa Polisi walikuwa akimuuliza kuwa gari amelitoa wapi, na je hakuiba sehemu. ‘Wiki iliyopita nilisimamishwa na Polisi wakati nikirejea nyumbani, Doncaster.”
”Na kila wakati walikuwa wakiuliza, gari hili limeibiwa ?, hili gari umelipata wapi ?Unafanya nini hapa ?, Unaweza kututhibitishia kuwa hili gari umelinunua wewe ?”
Rose ambaye alikwenda Newcastle kwa mkopo akitokea Spurs mwezi Januari, aliongeza kuwa hii imekuwa ikitokea kwangu tangu nilivyokuwa na umri wa miaka 18, tangu nilivyoanza kuendesha.”
”Hata nikipanda treni, kuna siku nikiwa na begi langu naingia kwenye treni, Wahudumua akaniuliza hivi unajua hapa ni ‘first class?”, nikamwambia ndiyo wakasema sawa tunaomba tuone tiketi yako.”
”Ghafla watu weupe wawili wakapita, nikamuuliza mbona hawa hujawaomba tiketi, akasema sawa haina haja.’
Rose akasema ”Baada ya hapo Polisi wakasema watani ripoti gari nilikuwa siliendeshi vizuri.”
Nyota huyo raia wa Uingereza anaingiza kiasi cha paundi 60,000 kwa wiki na alikuwa akiendesha gari hilo la Range Rover alilonunua kwa paundi 100,000 pia amesema namna alivyokuwa akijaliwa vibaya kutokana na rangi yake wakati alipokuwa ndani ya treni.
Comments