VIDEO:Tazama RC Makonda Alivyowatangaza Baadhi ya Mashoga...James Delicious Atajwa na Wengi

NancyTheDreamtz


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameunda Kamati ya watu 17 ya kuchunguza masuala mbalimbali yanayofanywa na baadhi ya vijana wa Mkoa huo kinyume na sheria na desturi za nchi ikiwemo ushoga na kurekodi video za ngono kisha kuzisambaza.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku tangu alipowataka wakazi wa Dar kumtumia majina ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo baada ya video ya msanii Amber Rutty kusambaa mitandaoni akifanya mapenzi kinyume cha maumbile.

“Kitendo cha kumuingilia mtu kinyume cha maumbile ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya taifa letu, lakini kuna watu wanajiuza kwenye mitandao na wanaona kwao ni jambo la kawaida, hii ni aibu kubwa.
“Mpaka sasa nimepokea meseji 18972, sio mchezo, wote wanalaani, majina 200 ni ya mashoga, mengine yanajirudia kama James Delicious, Dida Mtamu, Anti-Miliki na makundi ya ngono ya WhatsApp kama #PachuPachu wote wametajwa. Endeleeni kutuma meseji.
“Yupo kijana mmoja ni mtoto yatima, alichukuliwa na mzungu kumlea lakini akamgeuza kuwa mke wake, anamsomesha, na mpaka sasa anaendelea lakini kasema anataka kuacha, ndio maana tumeweka kitengo cha counseling kwenye kamati.
“Haya siyo maadili ya Mwafrika, tunakaribisha laana kwenye taifa letu, tunashangaa mambo mengi tunaomba lakini hayaendi, kumbe tunalaaniwa kwa vitendo ambavyo hakuna imani ya Kikristo wala Kiislam inayobariki mambo kama haya.
 “Ndugu zangu wa Haki za Binadamu, nafahamu hili jambo nilishawahi kuligusia kipindi cha nyuma, na Mataifa mengine ambayo yamepokea na kukubali ushoga, sisi tuna utamaduni wetu, tuna sheria zetu, msituingilie. Kama nyinyi mnaona mashoga ni haki, wachukueni mkakae nao kwenye nchi zenu, lakini kwenye mkoa wetu (Dar es Salaam) hatuhitaji mashoga, hakuna haki ya mashoga, kwa sababu sheria imebainisha.
“Tutawapima wote watakaotajwa majina yao kupitia kwa madaktari wetu, kuna mashoga wengine wanatambulika kwani wanatembea na Pampers na wanatoa harufu mbaya sana, yaani kifupi wameoza. Wanaume mtakaotajwa na mashoga kwamba mnashiriki, sheria imetaja wote wawili mnakwenda miaka 30 au maisha, kwa hiyo wote wawili watashitakiwa mahakamani. amesema RC Makonda.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele