Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Ligi Kuu Ubelgiji...Atupia Tena Mawili

NancyTheDreamtz
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta anazidi kuwa tishio kwa magolikipa katika michuano ya Ligi Kuu Ubelgiji na Europa League, usiku wa October 31 KRC Genk walikuwa ugenini kucheza game yao ya 13 ya Ligi Kuu Ubelgiji (Jupiter Pro League) dhidi ya Antwerp FC.

KRC Genk wakiwa ugenini licha ya kutanguliwa kwa magoli 2-0, walifanikiwa kusawazisha magoli yote na Mbwana Samatta akafunga magoli mawili ya ushindi dakika ya 76 na 90 baada ya Ruslan Malinovsky kuisawazishia Genk magoli ya mawili ya mwanzo kwa mikwaju miwili ya penati aliyofunga dakika ya 56 na 60, magoli pekee ya Antwerp yakifungwa na Bolingi dakika ya 23 na Jukleroed dakika ya 45.

Ushindi huo umeifanya Genk kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha jumla ya point 33 wakifuatiwa na Club Brugge waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 30, wakati Antwerp wapo nafasi ya tatu kwa kubaki na point zao 25, Samatta baada ya kufunga magoli hayo mawili sasa ndio anaongoza katika list ya wachezaji wanowania ufungaji bora, akifunga magoli 10 akifuatiwa na Ivan Santini wa Anderletch mwenye magoli 9 hivyo hadi sasa hakuna mchezaji anayemkuta Samatta kwa magoli.

Kwa ujumla magoli mawili ya Samatta aliyoyafunga yanamfanya awe na wastani wa kufunga kila game akiwa na KRC Genk msimu huu akiichezea game 23 za mashindano yote na kufunga magoli 23, pia akitoa assist 2, akifunga hat trick mbili na ameoneshwa kadi mbili za njano, kwa mujibu wa takwimu Samatta ameitumikia KRC Genk msimu huu kwa asilimia 85 katika game zote.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais