Sheikh Majini: Lissu Tumia Maneno ya Busara

MTABIRI na mtaalamu wa visomo na dua, Sheikh Sharrif Majini, amemtaka mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Tundu Lissu kupunguza ukali wa maneno katika hotuba zake anazozitoa kupitia mikutano yake.

 

Majini amesema hotuba iliyotolewa juzi Jumatano na Tundu Lissu haikuwa ya kizalendo na imejaa maneno yakuwagawa Watanzania na kuhatarisha usalama wa nchi.

 

Watanzania niwaelewa, wasikivu, pia wanaithamini sana amani waliokuwa nayo na kuitunza. Watashangaa sana wakiona kipindi hiki kabla ya kampeni kuanza anatokea mgombea na kusema kwamba akishindwa atawaingiza watu barabarani, tena akishawishi na vyama vingine viingie barabarani.

 

“Tunamsihi atumie maneno ya hekima na busara Watanzania watamuelewa. Kauli kama hizi ni hatari kwa Taifa letu kwa sababu tumeona mataifa mengi yameingia kwenye machafuko kwa kauli kama hizi, matokeo yake amani imechafuka katika mataifa hayo, amani imechafuka katika mataifa hayo na hakuna tena maelewano.

 

“Sasa kwa nchi yetu sisi Watanzania tunaomba viongozi wa dini wafanye maombi ya kutosha katika kipindi chote cha kampeni ili wanasiasa waovu wajulikane mapema,” alisema Sharrif.

 

Aidha, Majini ameviomba vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa wanasiasa ambao wanahatarisha masuala ya usalama.

 



NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele