Klabu ya Simba Yampa Tuzo Maalumu Diaamond Platinum Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

NancyTheDreamtz
Afisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara hapo jana amemkabidhi tuzo msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz kwa niaba ya klabu hiyo.


Manara amemkabidhi Diamond tuzo hiyo kwenye siku yake ya kuzaliwa hapo jana siku ya Jumanne mbali na zawadi hiyo amempatia keki yenye nembo ya Simba kutokana na msanii huyo kuwa shabiki mkubwa wa klabu hiyo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Manara amemwagia sifa msanii huyo kuwa ni mwanamuziki mkubwa ulimwenguni.

Branding ya kitu chochote kile haijengwi kwa kukaa ofisini peke yake na mifaili na milaptop kama ww ndio uliyeanzisha Microsoft..ni kutoka ktk events na matukio tofauti..maana ya media officer wa club ni zaidi ya publicity secretary..halaf Simba ikiongoza kwa mapato mtatafuta mchawi.. hv mnajua kwa Jay Zee na Rihana kujitangaza tu ufuasi wao kwa Arsenal nn walipata wajukuu wa Babu Wenger? Unadhani mm mjinga kutumia ushawishi wa kina.

Kwa kadri ilivyo ww ni Msanii na Mwanamuziki mkubwa c Bongo tu bali kote Ulimwenguni…Simba SC inatambua mchango wako ktk kukuza sanaa na kusaidia Soko la ajira kwa vijana,ikiwa ni pamoja na kuwa Owner wa @wasafitv..mbali ya hayo tunajua kwa ww kutumia nick name ya Simba ni kuzidi kutanua brand zetu mbili..cc kama klabu tunakukabidhi Tuzo maalum kwa hayo na keki yenye Simba ktk kuadhimisha Siku yako ya leo ya kazaliwa… Happy birthday Nassib Abdul..from Tandale uswahilini hadi kuwa Star Mkubwa Africa…

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele