Diamond kuwasaidia watoto 300, kina mama 200 Tandale ....Pia Kaahidi Pikpiki 20 Kwa Vijana wa Tandale

NancyTheDreamtz
Katika kusherekea siku yake ya kuzaliwa msanii Diamond Platnumz ameamua kufanya kitu cha kipekee zaidi.

Muimbaji huyo ambaye Birthday yake ilikuwa hapo jana, October 02, 2018 amepanga siku ya Ijumaa wiki hii kufanya tukio la kutoa misaada Tandale ambako ndipo amezaliwa.

"Jambo la kwanza kabisa ni kuzungumza na vijana wenzangu wa Tandale na kuwapa maneno fulani ya kuwaongezea moyo. Siku hiyo nitatoa bima ya afya kwa watoto sio chini ya 300," amesema.

"Vile vile tutakuwa tunatoa mitaji kwa wamama wasiopungua 200 wa pale Tandale kwa hiyo birthday yangu nitakuwa naisherekea hivyo," Diamond ameiambia Wasafi TV.

Pia Diamond ameongeza kuwa atatoa bodaboda 20 kwa vijana ambao hawana ajira pamoja na kukarabati baadhi ya shule hapo Tandale.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele