Jeshi la Uganda lazindua kondomu zenye kibwagizo ‘Usiende nyama kwa nyama’ kuwalinda wanajeshi wake

NancyTheDreamtz
Jeshi la Uganda limezindua mifuko ya kondomu katika kambi yake ya kijeshi ya UPDF Bombo iliyopewa kibwagizo cha usiende nyama kwa nyama. 
Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Brigedia Leopoldo Kyanda amesema mwanajeshi hawezi kutekeleza wajibu wake ipasavyo bila wenyewe kujilinda kutokana na maambukizi ya zinaa na hususan virusi vya ukimwi.
Kondomu hizo zimepewa jina Ulinzi na zinatarajiwa kusaidia katika juhudi za kupunguza kuenea kwa virusi vinavyosababisha Ukimwi.
Kitengo cha kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi jeshini kilizindua nembo hiyo mpya kwa ushirikiano na mashirika mawili yasiyo ya kiserikali.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele