MAHABA NIUWE: Kanye West amlipa Kim Kardashian Tsh bilioni 2 kulinda penzi lake

NancyTheDreamtz
Rapper Kanye West imemlazimu kumlipa mke wake Kim Kardashian kiasi cha dola milioni $1 ambayo ni sawa na Tsh bilioni 2 baada ya kumzuia mke wake kuposti picha moja ya tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Related image
Kanye West na Kim West
Kim akiwa kwenye mahojiano ya uzinduzi wa Podcast ya mtangazaji maarufu nchini Marekani,  Ashley Graham ‘Pretty Big Deal’, Kim amesema kuwa wiki moja kabla ya siku ya Mama duniani alitafutwa na kampuni kubwa ya mavazi nchini Marekani ikimtaka aposti picha moja ya tangazo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na itamlipa dola laki 9.
Kim amesema yeye aliona ni fedha nyingi lakini ilimpasa aombe ushauri kwa mumewe, lakini Kanye West akamkatalia kufanya hivyo.
Nilimpigia kuomba ushauri lakini akaniambia..’No babe, I really don’t want you to do that,’ nilipomuuliza kwanini? akasema kama unanipenda achana na hilo tangazo,“amesema Kim kwenye mahojiano hayo.
Hata hivyo, wiki mbele baadae May 12 mwaka huu siku ya Mama Duniani, Kanye alimtumia Kim maua na bahasha iliyokuwa na hundi (cheque) ya dola milioni 1 iliyoambatana na ujumbe uliosomeka “Nashukuru sana kwa kunisikiliza na kutoposti lile tangazo, nakupenda na nitakulinda kwa kila namna, furahia siku hii muhimu kwako“.
Ingawaje Kim hajaelezea sababu hasa ya kukatazwa kuposti tangazo hilo, lakini huenda isiwe ni ishu ya mahaba bali ikawa ni kutokana na ishu za kibiashara kwani na yeye ana bidhaa zake za mavazi za Yeezy.
Sikiliza interview yote ya Kim kwenye Podcast ya ‘Pretty Big Deal’

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele