Aunt Ezekiel Azungumzia Penzi Lake na Mose Iyobo

NancyTheDreamtz
Aunt Ezekiel Azungumzia Penzi Lake na Mose Iyobo
Msanii wa Filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuhusu maisha yake ya kimahusiano na Mose Iyobo ambaye pia ni dancer wa msanii Diamond Platnumz.

Aunt amesema kuwa wanapokuwa kwenye familia anasahau kabisa iwapo mumewe ni dancer kwani anapokuwa ndani anabeba majukumu kama baba.

"Huwezi kuamini kuna time nasahau kama ni dancer kwa sababu anaporudi nyumbani u-dancer anaacha njee, akifika ndani anakuwa baba, na hivi anavyosafiri ndio sijui kabisa kama anacheza au nini," Aunt ameiambia Wasafi TV.

Aunt Ezekiel na Mose Iyobo wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwae Cookie ambaye ni miongoni mwa watoto wanaofuatiliwa zaidi kwenye mtandao wa Instagram akiwa na followers zaidi ya laki nne.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele