Video: Aslay na Nay wa Mitego walivyopigana vikumbo Burundi

Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego pamoja na muimbaji Aslay wameonekana kufanya vizuri katika show zao mbili tofauti zilizofanyika weekend hii nchini Burundi. Kila mmoja akionekana kufanya vizuri zaidi baada ya kupost clips za video za shows.
Aslay alifanya show yake hiyo Bunyenzi Bunjumbura siku ya Jumamosi na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani mashabiki waliojitokeza ukumbini hapo walionekana kumshangilia kwa nguvu huku wengine wakilia kuonyesha ishara ya upendo.
“Abarundi mwarakoze kurukundo mwatweretse 🇧🇮🇧🇮🇧🇮,” aliandika Aslay.
Naye rapa Nay wa Mitego alikuwa nchini humo siku hiyo hiyo ya Jumamosi, na yeye alionyesha makeke yake mbele ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika show huyo.
Rapa huyo amedai hakuwai kuwaza kama anaweza kupata mashabiki wangi nchini Burundi
“BURUNDI BURUNDI BURUNDI. Mungu Awabaliki Sijawai Kuwaza Wala Kufikilia Kama Napendwa Kiasi Iki🙏🏿 Nje Ya Nyumbani Kiasi Cha Kujaza Uwanja. #OneManArmyShow✊🏿 Hakuna Wimbo Wangu Wasioujua wanaimba Kila Ngoma. Asanteni Sana Burundi. Next Stop CONGO✊🏿,” aliandika Nay wa Mitego.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais