Warembo Waliotikisa Ubunge Viti Maalum

 

KINYANG’ANYIRO cha kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana CCM (UV-CCM), kimeendelea kutikisa baada ya mchakato huo ulioanza mwishoni mwa wiki, kushuhudia sura mpya za walimbwende zilizoibua gumzo nchini.

 

Katika mchuano huo, wajumbe wa UVCCM katika kila mkoa, walipiga kura za maoni kuchagua wawakilishi wao, ambao watapata fursa ya kupeperusha bendera ya CCM baada ya uchaguzi mkuu kufi kia tamati Oktoba 28 mwaka huu.

 

Katika uchaguzi huo, mbali na wanawake hao kuwa na umri mdogo, lakini kivutio kingine kilichoibua mtikisiko wa kipekee katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ni urembo walionao washindi hao.

 

Baadhi ya wachangiaji katika mitandao hiyo, walihoji iwapo mojawapo ya vigezo katika nafasi hiyo ni kuwa mlimwende, jambo ambalo lilikanushwa na baadhi ya viongozi waliozungumza na IJUMAA Wikienda.

 

“Si kweli kuwa urembo ndiyo kigezo, cha msingi tunazingatia elimu kwa mujibu wa taratibu, uweledi na uzalendo kwa maana ya kuwa na uwezo wa kujieleza, kutetea hoja ili kuwakilisha wananchi wa mkoa fulani,” alisema mmoja wa wajumbe walioshiriki mchakato huo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Hata hivyo, baadhi ya wachangiaji katika mtandao wa Twitter, walisema ni dhahiri Bunge lijalo litakuwa na mvuto wa kipekee kutokana na mwonekano wa washindi hao wa kura za maoni kama watapitishwa na kushinda.

 

“Wajumbe! Hapo naona kila mkoa ni mwendo wa visu tu. Hakika bunge lijalo mambo yatakuwa moto, upinzani wataacha kususia vikao na kutoka nje,” alisema mmoja wa wachangiaji aliyejitambulisha kwa jina la Charles Nesphory.

 

Aidha, wachangiaji hao walionesha wasiwasi kuhusu vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kushamiri katika mchakato huo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James alionya jumuiya za chama hicho kutojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato kuelekea uchaguzi mkuu ili kuhakikisha viongozi watakaopatikana, wanakuwa bora.

 

“Kaeni macho na wagombea wanaoibuka katika maeneo yenu wakiomba uwakilishi wa ubunge na udiwani, huku wakigawa fedha ili wachaguliwe, waulizeni walikuwa wapi siku zote wakati mlipokuwa mnajinyima, mnahangaika usiku na mchana kukijenga chama na iweje waje sasa,” alisema James.

Kwa mujibu wa taratibu za CCM, baada ya washindi kupitishwa katika mchakato wa vikao vya juu vya chama hicho, majina yao yatawasilishwa katika Ofi si za Tume ya Uchaguzi (NEC) ambako nayo itawateua kulingana na idadi ya nafasi ambazo CCM itakuwa imeambulia katika majimbo na kura za urais.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilivuna wabunge 64 wa viti maalum, Chadema 36, huku CUF ikipata viti 10.

WASHINDI MIKOANI HAWA HAPA

Hadi kufi kia juzi, baadhi ya mikoa ilikuwa tayari imetangaza matokeo ya kura hizo za maoni, ambapo mkoa wa Morogoro mshindi alikuwa Rehema Nathan aliyepata kura 25 wakati mshindi wa pili akiwa ni mjasiriamali ambaye ni mmiliki wa Arabic Cakes, Warda Abdallah aliyepata kura nane.

Mikoa mingine washindi wa viti maalum CCM ni kama ifuatavyo; Iringa; ni Seki Kasuga mwenye kura 12 kati ya kura 27 zilizopigwa.

Mtwara; Mshihiri Mwanemo mwenye kura 17 kati ya kura 35 zilizopigwa.

Arusha; ni Lulu Mwacha mwenye kura 18 wakati nafasi ya pili ilienda kwa Tezra Semuguluka aliyepata kura 10.

Geita; ni Naomi Misungwi mwenye kura 15 kati ya kura 31 zilizopigwa.

 

Songwe; Mshindi wa kura za maoni CCM Ubunge Viti Maalum (Vijana) Songwe ni Fatuma Mnahwate mwenye kura 15 kati ya kura 27 zilizopigwa.

Mara; ni Juliana Didas Masaburi aliyepata kura 36 kati ya kura 38 zilizopigwa.

Pwani; ni Khadija Khalid Ismail aliyepata kura 15 kati ya kura 40 zilizopigwa.

 

Dar; Mshindi wa kura za maoni CCM Ubunge Viti Maalum (Vijana) Mkoa wa DSM ni Dorice Mgeta mwenye kura 10 kati ya kura 36 zilizopigwa.

Ruvuma; Judith Kapinga aliibuka mshindi wa kura za maoni CCM, upande wa Ubunge wa Viti Maalum (Vijana) Mkoa wa Ruvuma baada ya kupata kura 21 kati ya kura 34 zilizopigwa.

 

Kilimanjaro Agness Mchau naye aliibuka mshindi Mkoa wa Kilimanjaro katika kuwawakilisha vijana baada ya kupata kura 24, akifuatiwa na Lucy Ndosi aliyepata kura 7.

Kagera; Mbunge wa Viti maalumu aliyemaliza muda wake akiwakilisha Vijana Mkoa wa Kagera, Halima Bulembo aliongoza tena katika Uchaguzi wa kura za maoni CCM zilizopigwa juzi kwa kupata kura 35 akifuatiwa na Joanfaith Kataraia mwenye kura 9.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele