Meninah Apewa Makavu Laivu!

MSANII wa muziki, filamu na mshehereshaji maarufu BongoMeninah Attick, amepewa makavu laivu baada ya kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji na mwanaume.

 

Meninah aliposti video hiyo akifanyiwa masaji na mwanaume asiyejulikana, jambo ambalo liliwakera wafuasi wake waliosema kwamba, anarudia yaleyale ya mwaka jana.

 

Baadhi ya wafuasi hao walimshambulia kwa kusema kuwa mambo mengine anajitakia mwenyewe.

“Huyu mwanamke sijui huwa hajielewi? Anajirekodi mwenyewe video zake halafu anakuwa wa kwanza kukimbilia Polisi na kuwaletea shida watu wengine,” aliandika mmoja wa wafuasi wake anajiita Saraatz.

 

Oktoba 10, mwaka jana, Meninah aliitwa na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kuhusishwa na kosa la kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo lilimuingiza matatani mwigizaji na komediani Burton Mwemba ‘Mwijaku’ ambaye mpaka sasa ana kesi ya Makosa ya Mtandao.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele