Jide: Zuchu Atafika Mbali!

MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ amesema kuwa msanii na memba mpya wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’, atafika mbali kutokana na juhudi zake.

 

Akizungumza na OVER THE WEEKEND, Jide amesema, Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.

 

“Zuchu ana juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake, kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi (Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’ amesema Jide.


NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele