Shirika la WHO laonya kuwa janga la corona litachukuwa muda mrefu



Shirika la afya duniani WHO limeonya jana kuwa janga la virusi vya corona litadumu kwa muda mrefu na huenda likasababisha ''kulemewa kwa mikakati ya kukabiliana nalo'' huku India na Ufilipino zikiripoti ongezeko la maambukizi mapya.

Miezi sita baada ya shirika hilo la WHO kutangaza janga hilo kuwa dharura ya kimataifa, shirika la habari la AFP limeripoti kuwa virusi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 680,000 na maambukizi ya zaidi ya watu milioni 17.5.

Kamati ya dharura ya shirika hilo inayofanya tathmini mpya kuhusu janga hilo, imesema janga hilo linatarajiwa kuwa la muda mrefu na kutaja umuhimu wa kudumisha juhudi za kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa za kukabiliana na virusi hivyo.

 Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, shirika hilo la WHO limesema linaendelea kukadiria kiwango cha hatari cha kimataifa cha COVID-19 kuwa juu sana.
NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)