Dj Cuppy Amkubali Rayvanny!

MKALI wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny, ameendelea kupaa kimataifa baada ya kukubalika kinoma na DJ mrembo kutoka Nigeria, DJ Cuppy kumshirikisha kwenye Ngoma, Jollof On The Jet na staa mwingine wa nchini humo, Rema.

DJ Cuppy ameweka wazi kuwa katika ngoma hiyo iliyotoka juzikati ina mchanganyiko wa ladha za Afro- Pop na Afro-Beat huku Rayvanny na Rema ambao wote ni washindi wa tuzo za BET wakionesha uwezo mkubwa.

“Kufanya kazi kwa ushirikiano huu wa Rayvanny na Rema wa hapa Nigeria umenitia moyo, hii ni Afro-Pop iliyoboreshwa, japo hatujarekodi pamoja studio, lakini tumetoa ngoma kali ambayo naamini kila mmoja ataipenda hivyo naomba sapoto kutoka kwa mashabiki Afrika Mashariki,” amesema DJ Cuppy ambaye tayari amefanya kazi na mastaa kibao akiwamo Tekno na Zlatan.

DJ Cuppy alianza kujipatia umaarufu mwaka 2014 kwenye Tuzo za MTV Africa Music na mwaka uliofuata alifanya ziara yake ya Cuppy Takes Africa Tour ambayo iliwekwa kwenye makala ya Fox Life.

NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele