Magufuli apiga simu Tamasha la Nguvu ya Mwanamke


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tamasha la Nguvu ya Mwanamke (Girl Power), linatakiwa liwe endelevu ili liweze kusaidia kujua vipaji vya wasichana vinavyotakiwa kuendelezwa ili kufikia maendeleo ya taifa.


Amezungumza hayo leo Agosti 2, 2020 alipopiga simu wakati Tamasha likiendelea nakuongea na wanawake waliopo katika Tamasha hilo huku akiwapongeza na kueleza ni kwa jinsi gani amefurahishwa na tamasha hilo linalolenga kumjenga mwanamke.

"Nimefurahi kipindi hiki ni kizuri na kinatakiwa kiendelezwe ili kusudi tujue vipaji vya wasichana ambao tunatakiwa kuwaendeleza katika maendeleo ya taifa hili", amesema.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa wakina mama pamoja na wakinadada wa Tamasha hilo la Nguvu ya Mwanamke wanaweza na amefurahishwa nao sana.

“Ningetamani niwe hapo na nyie ila nimefurahi, tuko pamoja, siku nyingine na mie mnikaribishe tuwe pamoja, nipo pamoja nanyi, mmeninsipire sana mmefanya kazi kubwa kwa Taifa hili, Wanawake sitowaacha na sitowaangusha”.
NancyTheDreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele