Mrembo Huddah MonroeAkana Kumpa UTAMU Harmonize

NancyTheDreamtz

DAR: Siyo taipu yangu! Sosholaiti ambaye ni modo maarufu nchini Kenya ameibuka na kukana kumpa penzi staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ akidai eti siyo taipu yake.

Huddah ambaye ni shoga wa mzazi mwenza wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka hayo baada ya kupita muda mrefu tangu alipodaiwa kutembea na Harmonize au Harmo miaka kadhaa iliyopita.

Kupitia vyombo vya habari vya Kenya hivi karibuni, Huddah ameapa kuwa hajawahi kumvulia nguo ya ndani jamaa huyo kama wengi wanavyoamini.

Huddah amefunguka kuwa, video iliyosambaa miaka miwili iliyopita ikimuonesha akiwa kimahaba na Harmo ilikuwa nchini Afrika Kusini wakila bata.

Alisema kuwa, siku hiyo alikuwa na Zari ambaye wakati huo alikuwa mpenzi wa Diamond au Mondi ambapo walikuwa wamekaa pamoja ndipo wakajirekodi kipande hicho cha video na baada ya hapo kila mmoja aliendelea na hamsini zake.

Alisisitiza kwamba, si kweli kwamba walibusiana, bali watu ndiyo walitia chumvi kwenye video hiyo.

“Kusema kweli mbele za Mungu, Konde Boy (Harmonize) siyo taipu yangu. Tulikutana SA (Afrika Kusini), nilikuwa na Zari na Diamond, tulikuwa tunakula bata ndipo nikakaa naye na kupiga picha kisha biashara iliishia hapo,” alisema Huddah.

 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele