Rasmi Mbwana Samatta Aaga Genk na Kutimkia Uingereza

NancyTheDreamtz

MSHAMBULIAJI wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mtanzania, Mbwana Samatta amewaaga wachezaji na viongozi wa timu hiyo tayari kwa safari yake kwenda kucheza Ligi Kuu England ‘Premier League’.

 

Samatta anatajwa kuwaniwa na Norwich City inayoshiriki katika Premier ikidaiwa kuwa imeweka mezani dau la pauni milioni 11 (Sh bilioni 33).

 





“Samatta sasa hivi hayupo Ubelgiji ameshaaga wachezaji, viongozi na mashabiki juu ya suala la usajili wake wa kwenda kucheza England kwa sababu klabu zinazohitaji huduma yake ni nyingi.


“Unajua alitakiwa aondoke muda sana isipokuwa wakala wake wa awali alikuwa akimsubirisha na muda unapotea, baadaye ndipo akabadili wakala, ambapo tayari kuna ofa ya hao Norwich, pia kuna West Ham na Brighton ni jambo la kusubiria kuona itakuaje,” alisema mzee Samatta.

 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele