Makubwa..Wazazi Wamuua Mwalimu kwa Moto KISA Matokeo

NancyTheDreamtz


Imeelezwa kuwa mnamo Januari 6, 2020, nchini Kenya, wazazi walimshambulia mwalimu kwa moto hadi kupelekea umauti kwa madai kwamba wanalalamikia matokeo mabaya ya mtihani wa Darasa la nne.

Tume ya kuajiri walimu nchini Kenya (TSC), kupitia kwa Mkurugenzi wake, Nancy Macharia, imelaani kitendo cha baadhi ya wazazi hao kumshambulia na kumchoma moto mwalimu, Daisy Mbathe Mbaluka wa shule ya msingi Ndooni nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Januari 9 mwaka huu na Tume hiyo, imeamuru walimu Sita waliopo katika shule hiyo, kuondoka mara moja na kwamba haitoweza kupeleka tena walimu shuleni hapo hadi pale itakapohakikishiwa usalama wao kwanza.

Aidha taarifa zinaeleza kuwa tayari watu wawili wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho wamekwishakamtwa.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele