Waziri Mabula Aitaka Bodi Ya NHC Kupitia Upya Gharama Za Nyumba Inazouza
NancyTheDreamtz
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameitaka Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia upya gharama
za nyumba zake ilizojenga maeneo ya pembezoni kwa ajili ya kuziuza.
Dkt
Mabula alitoa kauli hiyo jana wilayani Masasi mkoa wa Mtwara wakati
alipotembelea mradi wa nyumba 54 zilizojengwa na Shirika la Nyumba la
Taifa akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi
katika mikoa ya Kusini pamoja na kutembelea miradi inayofanywa na NHC
katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli
hiyo ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafuatia
kulalamikiwa na wabunge wa Majimbo ya Masasi Dkt Rashid Chuachua na yule
wa jimbo la Lulindi mkoani Mtwara Jerome Bwanausi kuwa pamoja na
halmashauri kuhitaji nyumba kwa ajili ya watumishi lakini gharama
imekuwa kubwa kiasi cha halmashauri na wananchi kushindwa kuzinunua.
‘’
Ni vizuri bodi ikae iangalia namna ya kupitia upya gharama za nyumba
zote zilizopo maeneo ya pembezoni kama hizi za Masasi maana zikiachwe
bila kununuliwa itakuwa ni hasara’’ alisema Dkt Mabula.
Naibu
Waziri Mabula alisema, hata kama nyumba hizo zilizojengwa kwa ajili ya
kuuza hazitanunuliwa basi NHC iangaliae namna ya kuzipangisha na kueleza
uhitaji wa nyumba katika eneo la Masasi upo na watumisi wa serikali
wanahitaji kuisha maeneo rafiki.
Hata
hivyo, amezitaka halmashauri nchini kulitumia Shirika la Nyumba la
Taifa kujenga miradi ya nyumba za watumishi kulingana na mahitaji ili
kuepuka kujenga nyumba ambazo mwisho wa siku zinaweza zisinunuliwe.
Kwa
upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano
Saguya alisema shirika lake liko katika hatua za mwisho za kukamilisha
mradi huo uliokuwa umesimama kwa muda ambapo takriban milioni 600
zitatumika kuukamilisha na kusisitiza imani yake katika kipindi cha
miezi sita ujenzi utakamilika.
Kwa
mujibu wa Saguya, bei inayolalamikiwa ya shilingi milioni 54 kwa nyumba
moja inatokana na gharama kubwa iliyotumiwa na Shirika la Nyumba la
Taifa kuzijenga nyumba hizo na kubainisha kuwa NHC iko mbioni
kuzipangisha baadhi ya nyumba ambazo wananchi wameonesha nia ya kupanga.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt
Angeline Mabula alizitembea wilaya za Nanyumbu na Tunduru na kukagua
utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya hizo.
Dkt
Mabula alibaini utunzaji mbovu wa kumbukumbu za majala ya ardhi pamoja
na kiasi kidogo cha makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia kodi ya
ardhi ambapo aliziagiza halmashauri za Nanyumbu na Tunduru kuongeza kasi
ya makusanyo ya kodi ya pango la ardhi sambamba na kuzingatia utunzaji
majalada ya ardhi kwa kufuata taratibu ikiwemo kuwepo mawasiliano katika
majalada hayo kutoka afisa mmoja kwenda kwa mwingine.
Comments