NancyTheDreamtz Mnada wa kuuza korosho wilayani Newala na Tandahimba, Mkoa wa Mtwara umevunjika. Ulivunjika jana mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Omary Mgumba baada ya wakulima kukataa kuuza korosho ghafi katika mnada wa wazi wa kwanza uliofanyika Kijiji cha Makukwe, Wilaya ya Newala. Wakati wa mnada huo kulikuwa na kampuni 15 zilizotuma zabuni za kununua korosho ghafi kwa bei ya juu ya Sh 2,717 kwa kilo moja na bei ya chini ikiwa ni Sh 1,711. Wakati wanunuzi hao wakitaka kununua kwa bei hiyo, msimu uliopita katika mnada wa kwanza, kilo moja ya korosho ilinunuliwa kwa Sh 3,850. Pamoja na hali hiyo, ununuzi wa korosho mwaka huu wanunuzi wanatakiwa kufika wenyewe katika minada wakiwa na barua za zabuni tofauti na misimu iliyopita ambayo walikuwa wakipeleka barua katika vyama vikuu na kusubiri minada. Akizungumza baada ya wakulima kukataa kuuza korosho zao, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gellasius Byakanwa, aliwapongeza na kusema wamefanya uamuzi sahi...