Kusini Kivipi tutakwepa Hili Wanafunzi wa chidya wachoma moto Shule

NancyTheDreamtz
Kama kunaumasikini unaoutesa Mkoa wa Mtwara ni Elimu kwani kirekodi za matokeo huwa sio mzuri kiujumla Leo unakuta Shule ambayo inasifa kubwa Mkoani Mtwara Wilaya ya Masasi Chidya
wamediriki kuleta Mgomo kwakuchoma ofisi ya taaluma moto kama mtakavyojionea hapo chini ni aibu sana kusini wapi tunaelekea katika kuhakikisha tunaondoa aibu ya elimu duni.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Chidya iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefanya fujo na kusababisha uharibifu wa mali za shule na walimu wakidai walimu wanawabana sana kwenye masomo wakati wenyewe wanataka uhuru wa kutembea sio kuwa bize na masomo kila wakati.

Katika vulugu hizo wanafunzi walichoma pikipiki mbili, kuharibu vitu vyote ikiwemo tv, vitanda na vyombo vingine kwenye nyumba ya mwalimu wa taaluma pamoja na kuiba kuku 20 za mwalimu.
Kutokana na Vulugu hizo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa aliyefika shuleni hapo kujionea hali halisi, alieleza kuwa sababu iliyowafanya wananfunzi hao kufanya fujo inaonesha hawajitambui kabisa maana serikali itajitahidi kuboresha mazingira ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kuleta walimu lakini cha kushangaza wanasema wanafundishwa mno, ni jambo la ajabu sana.








Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele