Hafla ya Wabunge Yafana.... Wachangisha Mill. 800 Kwaajili ya Ujenzi wa Vyoo

NancyTheDreamtz
Hafla ya Wabunge yafana wachangisha Mill. 800
Takribani shilingi milioni 800 zimepatikana katika Hafla Maalum ya kuchangisha fedha kusaidia ujenzi wa vyoo vya watoto wa kike mashuleni iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam usiku wa jana.



Mgeni rasmi Spika Mstaafu Mama Anna Makinda akipokea mfano wa hundi kutoka kwa taasisi mbalimbali ambazo zimechangia Fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo kwa watoto wakike mashuleni.



Mbunge wa Mbulu Vijijini mhe;Flatey Maasai akiongoza jopo la wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuruka sarakasi na kuendesha baiskeli ya tairi moja jukwaani na mhe; Vicky Kamata Mbunge wa viti maalumu akaongoza kwaya(choir) ya bunge,lakini singeli ikasimamiwa na mhe;Ali Ungando mbunge wa Kibiti ni katika hafla ya kuchangia  ili mtoto wa kike aweze kupata choo bora





Wabunge wakiburudika kwenye hafla ya kuchangia  ili mtoto wa kike aweze kupata choo bora iliyofanyika Mlimanin City, jijini Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele