Ali Kiba Apewa Zigo la Mabao Coastal Union

NancyTheDreamtz

Mshambuliaji wa Coastal Union, Alli Salehe ‘Alikiba’ ni kama amepewa zigo la mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kocha wa kikosi hicho, Juma Mgunda kumtaka afunge zaidi ya mabao 25 kwa kile alichodai uwezo wa kufanya hivyo anao.

Alikiba tangu asajiliwe na timu hiyo msimu huu, bado hajaoneka­na uwanjani wakati tayari wenzake wameshacheza mechi mbili mpaka sasa na leo Jumamosi wanatarajiwa kupambana na KMC katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa.

“Mashabiki wa Coastal Union wa­nachotakiwa kufahamu ni kwamba timu hii imesajili wachezaji 30 na kila mchezaji anataka kucheza, hivyo muda ukifika kila mmoja ataonekana uwanjani.

“Najua wengi wanamuulizia Alikiba, niseme tu ataonekana uwanjani muda si mrefu na niwaambie ni mshambulia­ji mzuri na anaweza kufunga zaidi ya mabao 25 msimu huu,” alisema Mgun­da.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele