Cheyo: “Vijana Njooni Niwajaze Mapesa”

NancyTheDreamtz

Mwenyekiti wa UDP taifa John Cheyo amefunguka kuwa hawezi kuhama chama alichokianzisha mwenyewe na kuhamia CCM, na kuwataka vijana kujiunga na chama chake ili wajipatie pesa.

Cheyo ambaye ni maarufu kwa jina la Bwana Mapesa amefunguka hayo kupitia Weekend BreakFast leo Jumamosi Septemba mosi, ambapo amesema kuwa siasa za upinzani zikiendelea hivi kwa viongozi wa upinzani kuhama na kupandikiza chuki wapiga kura hakutakuwa na mtu wa kumtoa Rais Magufuli madarakani.

“Siwezi hama chama kwenda kuunga jitihada ntaunga nikiwa UDP siwezi hama nyumba yangu mimi ndio baba mwenye nyumba, nawakaribisha vijana na wote wenye mapenzi na siasa waje kwangu UDP niwajaze mapesa”, amesema Cheyo.

John Cheyo ni moja ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini akiwa mwanzilishi wa Chama cha United Democratic Part (UDP).

Cheyo alipata umaarufu sana nchini katika kinyanganyiro cha uchaguzi cha mwaka 2005, ambapo alisema kwa ufupi kwamba sera zake ni "kuwajaza watanzania mapesa". Hii ilikuwa ni sera inayopendwa sana na watu kwa sababu wakati huo baadhi ya watu walikua wanalia hali ngumu ya maisha.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele