Simba Yafungua Ligi Vizuri Yaitandika Tanzania Prison Bao 1-0

NancyTheDreamtz
Simba Yafungua Ligi Vizuri Yaitandika Tanzania Prison Bao 1-0
MABINGWA watetezi, Simba wameanza vizuri Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Tanzania Prisons ya Mbeya bao 1-0 katika mchezo uliofanyika usiku huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Bao la Simba limefungwa na mshambuliaji kutoka Rwanda, Meddie Kagere aliyefunga dakika ya pili kwa shuti kali baada ya kupewa pasi na John Bocco kutoka upande wa kulia.


Kikosi cha Simba: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dillunga/Nicholas Gyan dk82, Meddie Kagere, John Bocco/Adam Salamba dk83 na Shiza Kichuya/Muzamil Yassin dk67.


Tanzania Prisons: Aaron Kalambo, Benjamin Asukile, Laurian Mpalile, Nudrin Chona, James Mwasote, Jumanne Elfadhili, Salum Kimenya, Cleophace Mkandala, Kelvin Friday/Lambert Sabiyanka dk82, Salum Bosco/Ramadhani Ibata dk71 na Ismail Aziz/Hassan Kapalata dk79. 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele