Idriss Aamua Kupita Njia za Daimond Baada ya Kuwa na Wema Sasa Atoka Kimapenzi na Lynn

NancyTheDreamtz
Idriss Aamua Kupita Njia za Daimond Baada ya Kuwa na Wema Sasa Atoka Kimapenzi na Lynn
Msanii wa Bongo movie na comedian maarufu Idris Sultan anadaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Ex girlfriend wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kumekuwa na tetesi kuwa Video vixen ambaye hakauki vituko Kwenye mitandao ya kijamii Irene Geofrey maarufu kama Lynn ana banjuka na Idris Sultan.

Tetesi za Mahusiano ya wawili hao zilianza juzikati ambapo watu wengi walipigia mstari baada ya mwanadada huyo kuposti picha ya Idris huku akiandika maneno ya kimahaba yalisomeka; “Babyboo baby boo bae.”

Baada ya Tetesi hizo kupamba moto Kwenye mitandao ya kijamii gazeti la Risasi Vibes, lilimsaka Lynn ambaye mara moja alikana kuwapo kwa Mahusiano hayo:

Unajua muda mwingine unaweza kuposti kitu halafu maneno yakajiandika yenyewe, sasa ndicho kilichonitokea na mimi sikutaka kufuta kwa sababu watu wangesema ni kiki.

Lakini Idris ni mshikaji wangu wa karibu sana na ninampenda anavyochekesha, watu wasinitengenezee mambo ambayo hayapo jamani“.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele