Seebait.com 2018SeeBait Rapper 50 Cent Amsifia Nick Minaj Licha ya Kuchanwa Vibaya na Mrembo Huyo

NancyTheDreamtz

Rapper 50 Cent amekuwa wa kwanza kujibu kati ya male rappers kadhaa waliochanwa kiutani na Nicki Minaj kwenye wimbo wake wa hivi karibuni 'Barbie Dreams' kutoka kwenye album ya QUEEN.

Kwenye mahojiano na 'Extra' kupitia Hip Hop N More, 50 Cent ameweka wazi hisia zake juu ya wimbo ule kwa kuupa alama 100. Alisema: "Nimeupenda ule wimbo, niliwahi kufanya wimbo unaitwa 'How to Rob' na aliwahi kusema mwenyewe (Nicki Minaj) kuwa alivutiwa nao sana." alisema 50 Cent na kumsifia Nicki kwa uandishi wake wa mtindo wa mtazamo tofauti yaani kinyume (reverse perspective)

Aliongeza pia kuwa 'Barbie Dreams' inaonesha wazi kabisa kuwa wanawake kwenye Hip Hop wameanza kuchukua nguvu kutoka kwa wanaume - Swipe kuona interview hiyo.

Kwenye dude hilo, 50 Cent alichanwa kwenye line isemayo: "I tried to fk 50 for a powerful hour, but all that ni*a wanna do is talk 'Power' for hours." alichana Nicki.

Wengine waliotajwa kwenye wimbo huo ni Drake, Meek Mill, DJ Khaled, na wengine kibao.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele