Breaking News: Bobi Wine Akamatwa Tena Muda Mfupi Baada ya Kuondolewa Mashtaka

NancyTheDreamtz
Breaking News: Bobi Wine Akamatwa Tena Muda Mfupi Baada ya Kuondolewa Mashtaka
Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amekamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini.

Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Comments

Popular posts from this blog

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jeshi la Uganda lazindua kondomu zenye kibwagizo ‘Usiende nyama kwa nyama’ kuwalinda wanajeshi wake