Ray C "Wabongo Mitandaoni Wanapenda tu Vitu vya Kijinga vya Maana Holla"

NancyTheDreamtz

Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Ray C amedai kwamba asilimia kubwa ya watanzania hawajui kuitumia mitandao ya kijamii ipasavyo ili iwaingizie fedha, na badala yake wanaitumia kwa kujadili mambo yasiyo na tija kwa mtu mwenyewe na taifa kwa ujumla.

Ray C ameeleza hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv hii leo Agosti 23, 2018, na kusema watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha zao kuingia kwenye mitandao hiyo bila ya kufikiria ni jinsi gani itaweza kuwarudishia faida.

"Watu wengi mitandaoni wanapenda upuuzi, ukiweka kitu cha maana hakuna mtu ambaye ata 'comment' chochote katika hicho ulichokiweka, maana wanakichukulia poa lakini fanye kinyume chake hapo ndio utawajua walipo. Wenzetu Ulaya mitandao ya kijamii kama wakina Kim Kardishian na wengine wanatumia mitandao hiyo kuuza 'product' na kuonyesha kazi zao ili wapate pesa...

lakini sisi ndio tumekuwa wakutoa pesa kwa kununua bando ili tukaharibu, tena sana sana Tanzania hatujui kutumia mitandao ili itunufaishe na badala yake tunatumia kwenye upuuzi", amesema Ray C.

Mbali na hilo, Ray C amedai hasumbuki na maneno ambayo amekuwa akizungumziwa kwenye mitandaoo ya kijamii kwa kuwa ana wafahamu watanzania vizuri jinsi walivyo.

"Huwezi kuzuia watu kuongea wanachokifikiria, Nikiingia kwenye mitandao ya kijamii siendi tu kukurupuka na kuweka kitu chochote bila ya kuwa na uhakika wa jambo fulani. Lakini wenye akili pungufu wanaweza wasinielewe ninachokizungumza ila wale wenye akili timamu watakuwa wananielewa", amesisitiza Ray C.

Kauli hizo za Ray C zimekuja baada ya siku za hivi karibuni kushambuliwa kwenye mitandao ya kijamii, baada ya yeye kuonekana kimbele mbele katika kila jambo licha ya kutokuwa muhusika katika hilo, na kufanya watu wadai pengine anatafuta kiki ili aweze kuendelea kuwa gumzo kwenye midomo yao.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais