Daimond, Rich Mavoko Wakutana Uso kwa Uso Basata

Daimond, Rich Mavoko Wakutana Uso kwa Uso Basata
MKURUGENZI wa Kampuni ya WCB, ambaye pia ni staa wa Bongo Fleva, Nasbu Abdul  ‘Diaomond Platnumz’ na Mameneja wake wawili, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Sallam Sharraf wametinga katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuitikia wito wa baraza hilo kuhusu malalamiko yaliyowasilishwa na mwanamuziki Rich Mavoko aliyedai kuwa mkataba wake na WCB ni wa kinyonyaji.
Akizungumzia hilo mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo ya kutatua jambo hilo na kufikia mwafaka.
Sallam amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji. 

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele