Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais
NancyTheDreamtz Msanii wa filamu za Bongo Movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kudai anatamani sana kama angetoa Penzi lake kwa Raisi. Wolper amedai anaona ni bora kama atakuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa sasa statute Penzi pa Raisi yoyote Afrika kwani atakuwa salama zaidi kuliko kufaidi Penzi na wadananda wengine. Kwenye mahojiano na Global Publishers, Wolper alisema mara nyingi amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume ambao mwishoni wanamsaliti jambo ambalo halipendi na linamkera, lakini anaamini akimpa moyo wake wa upendo Rais yeyote Afrika anaona atakuwa salama. Unajua ndoto yangu mimi ningependa kutoa penzi langu kwa Rais maana najua kabisa, kwanza atakuwa ananiheshimu na itakuwa ni ngumu sana kunitenda kama wafanyavyo wengine na hapo nitatulia kabisa wala sitakumbuka wanaume wazugaji“. Wolper amekuwa muwazi kuhusu maumivu anayokutana nayo Kwenye mapenzi yake ambapo uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Harmonize uliisha baada ya kum...