Waziri Simbachawene aruhusu Polisi kuhamia nyumba mpya Dar





Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, George  Simbachawene ameruhusu askari wa polisi na maofisa wa jeshi hilo kuanza kuishi katika nyumba za kisasa za maghorofa pacha 11 na 23 zilizopo maeneo ya Mikocheni na  Kunduchi wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Mradi wa nyumba hizo ambazo familia 330 zinaweza kuishi, ujenzi wake ulikamilika miaka mitatu iliyopita lakini hazikuanza kutumika kwa sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kisera.

Simbachawene ametoa ruhusa hiyo leo Ijumaa Julai 9, 2021  alipotembelea mradi wa nyumba hizo zilizojengwa  na kampuni ya Mara World Tanzania Ltd.

Katika maelezo yake, Simbachawene alimuagiza mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( IGP), Simon Sirro kuhakikisha askari hao waingia mara moja katika nyumba huku taratibu za kisheria zikiendelea kutatuliwa kati ya Serikali na mwekezaji.

Uamuzi huo ulipokelewa kwa furaha na IGP Sirro ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa akiiangukia Serikali kuruhusu nyumba hizo kuanza kutumika ili askari watekeleze majukumu yao kwa ufanisi.

nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele