Mke wa Ben Pol Afunguka Mazito



Wakati bado kuna sintofahamu juu ya ndoa yake na staa wa RnB Bongo, Ben Pol, mrembo tajiri wa Kenya, Anerlisa Muigai ametoa ujumbe mzito juu ya uhusiano wake wa kimapenzi.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Anerlisa ameandika; “Ukianza kitu, kuwa na ujasiri wa kumaliza pia. Mimi siyo mama wa mtoto wa mtu, kwa hivyo usifikirie unaweza kushikilia maisha yangu…”

Kwa mtazamo wa mambo, Anerlisa anaweza kuwa anazungumzia kesi yake ya talaka na Ben Pol ambaye ni mumewe wa zamani.

Wakati habari za talaka yao zilipoibuka, ilisemekana kwamba Ben Pol ndiye aliyeanzisha taratibu za talaka.

 

Kupitia mitandao ya kijamii, mwanadada huyo alisema kwamba alichotakiwa kukifanya alishakifanya na ametia saini.

Alisema kwamba, jambo la muhimu maishani mwake sasa ni kazi yake na amani katika maisha yake.

 

“Nataka kuweka mambo wazi kuwa nilisaini chochote  kilichohitajika kusainiwa, na sitamani kuhusishwa na mtu yeyote mtazamo wangu hivi sasa, ni kazi yangu na amani yangu,” alisema Anerlisa .

Swali ambalo limesalia akilini mwa wengi ni je, kuna shida ambayo imeibuka kati ya Anerlisa na Ben Pol?

nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele