Timu ya kushabikia Katika fainali ya EURO 2020



Italia au England ni nani atainua kombe hilo Katika fainali ya UEFA EURO 2020 kwenye Uwanja wa Wembley mnamo Julai 11?



Je! Unatafuta timu ya kuishabikia katika michuano hiyo ya fainali? Au unatafuta timu ya kitaifa iliyo na wachezaji kutoka klabu unayoipenda?

Ikiwa unatamani kushabikia timu ambayo itaendana na mawazo yako, soma mwongozo wetu kwa waloingia fainali.

Uingereza

Ikiwa unapendelea sana Magoli basi Uingereza ni chaguo linalokufaa kutokana na magoli ambayo wameyafunga katika kufuzu kwao.

Vijana hawa wa  Gareth Southgate pia wanacheza EURO yao ya kumi na ndio timu ya taifa iliyocheza sana katika michuano hiyo ya EURO bila ya kunyakua taji hilo. je! Wakati wao umefika wa kunyakua taji hilo kwa mara ya kwanza tangu Kombe la Dunia la FIFA mnamo 1966?



Italia

Unafurahishwa na mchezo wa mikwaju ya penati? Ikiwa ndivyo, Italia ndio timu inayokufaa kwani wamehusika katika rekodi ya mafanikio makubwa sana katika upande wa penati ikiwemo ushindi wao wa nusu fainali dhidi ya Uhispania.

Mikutano yao iliyopita

• Timu hizo zimekutana mara 27, Italia ikishinda mara 11,England mara nane na huku wakipata sare nane.

• Italia ilishindwa kushinda mechi zote nane za mwanzo timu hizo zilivyoanza kukutana huku England ikishinda  katika mechi saba.

• Italia haijawahi kupoteza dhidi ya England kwenye fainali. Mfano mzuri ni ule ushindi waliopata wa 2-1 katika  fainali ya Kombe la Dunia la FIFA mnamo 1990.



Je! kulingana na moano yako, unahisi ni timu gani kati ya hizo mbili itachukua ubingwa wa EURO 2020?

nyandichethedreamtz

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele