Yanga yatoa sababu kubwa sita zakuifunga Gwambina leo

NancyTheDreamtz

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela  amesema kuwa wana sababu kubwa sita zinazowafanya washinde leo mbele ya Gwambina mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo saa 10:00 Uwanja wa Uhuru mshindi atakayepenya leo anatinga hatua ya robo fanali.

Mwakalebela amesema:-" Tuna kila sababu ya kuifunga Gwambina kwa sababu tuna benchi la ufundi zuri, wachezaji imara, mbinu kali, uwezo mkubwa, nia ya kufanya vizuri ipo.

"Pia kuifunga Gwambina kutaturejesha kwenye mstari wetu ambao tulikuwa kwani hatukuwa na matokeo mazuri  na itatufanya turudishe imani kwa mashabiki wetu hivyo ushindi wetu mbele ya Gwambina ni muhimu mashabiki mjitokeze kwa wingi," amesema.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele