Fahamu Kinachojiri Kuhusiana na Kirusi cha Corona (Coronavirus)

NancyTheDreamtz

Karibu kwa ajili ya kujuzwa na pia kupata taarifa (masasisho) mbalimbali ya kile kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus) almaarufu kama "kirusi cha Wuhan" kutoka nchini China.

Katika uzi huu utapata kufahamu mambo mbalimbali hususani hali ya ongezeko na ukuaji, jitihada zinazofanyika kukabiliana na kirusi hiki na mengine mengi yanayoibuka duniani kote katika muda wowote kuanzia sasa.

Nikukaribishe sana!

Coronaviruses in virusi vinavyopatikana zaidi kwa wanyama, lakini katika matukio machache virusi hivyo ninavyoitwa Zoonotic, Kisayansi, vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

Virusi hivi vinaweza kuwafanya watu wakaugua, mara nyingi katika sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji sawa kabisa na mafua ya kawaida.

Virusi husambaa kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine kwa njia ya hewa kwa kukohoa au kupiga chafya, kugusana na mtu mwenye virusi hivyo.

Njia nyingine ni kugusa kitu au sehemu yenye virusi na kisha kujigusa mdomo, pua au macho kabla ya kunawa na mara chache huambukiza kupitia kinyesi.

Dalili za kuwa umepata virusi hivi ni pamoja na pua kudondosha mafua mfululizo, kuumwa kichwa, kukohoa, kupata homa na muwasho katika koo ila kwa wenye kinga ndogo ya mwili kama wazee au watoto wanaweza kupata Nimonia (Pneumonia).

Hakuna Kinga ya virusi hivyo kwa sasa, ila usambaaji wake kwa binadamu unaweza kupunguzwa kupitia kuosha mikono yako mara kwa mara kwa maji na sabuni na epuka kugusa macho, mdomo na pua kwa mikono isiyooshwa.

Pia, unaweza kupunguza usambazaji wake kwa kukaa mbali na mtu aliyethibitika kuwa na maambukizi. Ukianza kuona dalili hizo unashauriwa kumuona daktari.

Ukithibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, funika mdomo na pua yako wakati wa kupiga chafya au kukohoa na safisha sehemu au kitu ulichokigusa.

Kirusi hiki cha Corona, kinaaminika kuwa kilianza katika soko la bidhaa za baharini mwishoni mwa mwaka 2019, katikati ya Jiji la Wuhan, China ambalo lilikuwa linauza nyama ya porini.


Kirusi hicho ni sehemu ya familia ya kirusi corona ambacho kinauhusiano na virusi vya SARS na MERS ambavyo vilisababisha milipuko siku za nyuma.

Kirusi hiki kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, pia katika maeneo mengine duniani kama Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, Malaysia, Vietnam, Taiwan, Singapore, Nepal, Macau, Hong Kong na Canada.

Mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kuwa, idadi ya watu wapatao 2045 wamegundulika kuwa na kirusi hiki huku wapatao 633 wakipatikana kwa siku ya jana pekee.

324 kati ya hao 2045 wako katika hali mbaya zaidi (critical condition) huku idadi ya waliokufa kutokana na kirusi hicho ikifikia 56 nchini China.

Hapo awali, China ilitoa tahadhari kuwa kirusi hiki kinaweza kusambaa kwa watu wengi zaidi.

Waziri wa Kamisheni ya Afya ya Taifa nchini China, Ma Xiaowei, akizungumza na vyombo vya habari, alisema kuwa, uwezo wa serikali wa kufahamu kirusi hiki kipya ni finyu na hawajui hatari zinazoweza kuambatana na kubadilika kwa kirusi hiki. [VOA]

Ma Xiaowei alisema muda ambao kirusi hiki cha corona huchukuwa hadi kujitokeza ni kati ya siku mmoja hadi 14, na kuwa kirusi hiki kinaambukiza hata wakati kinajijenga mwilini, kitu ambacho kilikuwa tofauti kwa homa kali ya mafua, SARS, kirusi corona kilichoibuka China na kuua takribani watu 800 duniani mwaka 2002 na 2003.

Mpaka sasa juhudi zilizokwisha kufanyika ili kudhibiti kuenea kwa kirusi hiki ni pamoja na katazo la usafirishaji na kusafiri na kusitisha matukio ya sherehe kubwa. China imetoa makatazo kadhaa ya kusafiri katika maeneo yaliyoathiriwa vibaya sana katika nchi hiyo ili kuzuia kuenea kwa kirusi hicho.

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)