Jacqueline Wolper Atuhumiwa Kuiba Mwanaume wa mtu

NancyTheDreamtz

Mtanzania anayetoka na mzungu aliyempita miaka 32 Azzy Super amesema msanii Jacqueline Wolper alimuibia mwanaume wake wa zamani ambaye ni msanii wa HipHop Lord Eyes.


Azzy Superstar ameiambia EATV & EA Radio Digital, wakati Jacqueline Wolper anatoka kwenye mahusiano na aliyekuwa mwanaume wake Lord Eyes, alikuwa anampiga vijembe kwenye mtandao wa Instagram kwamba atafute wa saizi yake.

 "Nilikuwa naishi na Lord Eyes Arusha, tulivyofika Dar es Salaam baada ya kupendeza ndiyo akaanza kutoka na Wolper mimi akaniacha kisa sio levo zake, kipindi wapo kwenye mahusiano Wolper alikuwa ananirushia vijembe kwenye mtandao wa Instagram ambavyo vilikuwa vinanilenga mimi kwamba nipambane na hali yangu" ameeleza Azzy Superstar.

 "Wolper alikuwa anampigia simu binamu yangu kwamba niachane na Lord Eyes na nisijifanye kama mimi ni mtu wangu ili wao waendelee na mapenzi yao, yeye ni dada wa mjini anafanya anayoyafanya" ameongeza.

Aidha amesema kitu anachojutia kwa Lord Eyes ni kupoteza muda wake na pesa juu ya kumsaidia kipindi alipokuwa soba

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele