Ndugai Akerwa na Kiongozi wa Serikali Aliyesema Mbele ya Rais Kuwa Wabunge Wamewadhihaki Wachezaji wa Taifa Stars
NancyTheDreamtz
Spika
wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kiongozi mmoja wa Serikali
aliyezungumza maneno yasiyofaa kuhusu Bunge la Tanzania na wabunge na
kumdanganya hadharani Rais John Magufuli kuwa wawakilishi hao wa
wananchi wamewadhihaki wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’, hajitambui.
Spika
ametoa kauli hiyo bungeni jana Juni 25, baada ya Mbunge wa Kigoma
Mjini Zitto Kabwe, (ACT-Wazalendo), kuomba muongozo kwa kutumia kanuni
ya 68 (7), kuhusu jambo lililotokea mapema bungeni.
Zitto
alilazimika kuomba muongozo huo baada ya Spika Ndugai kutoa ufafanuzi
kwamba hakuna mbunge yeyote aliyewadhihaki wachezaji wa Taifa Stars
baada ya mchezo wake na Senegal.
“Mheshimiwa
Spika, kwa kutumia kanuni 68 (7), kuhusu jambo lililotokea bungeni
mapema, umeelezea jambo ambalo limetokea nje ya bunge kuwa mmoja ya
viongozi wa serikali kuwabagaza wabunge waliokwenda Misri.
Mara baada ya mbunge huyo kuomba muongozo huo, Spika Ndugai, alijibu akisisitiza kuwaomba wabunge kutolikuza jambo hilo.
“Naomba
tusilikuze jambo hili kabisa, kama wabunge tungekuwa na mawazo kama
wachezaji wanamakosa isingewezekana wabunge wengine 30 kwenda Misri. Ni
bahati mbaya sana, kwamba tuna viongozi wa serikali, wanadiriki
kumdanganya Rais hadharani.
“Kiongozi
wa serikali unapoongea mbele ya Rais, jipange, ongea ukweli mtupu mbele
ya Mwenyenyezi Mungu na sisi hatutamani kusema, natamani kufunguka
kidogo…inatosha..inatosha.
“Nasema
wazi bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi kwa sababu ana
nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao ambao wanaweza
kumtukana Spika, lakini tuache,”alisema.
Comments