Baadhi ya Wabunge Kenya wamuunga mkono Jaguar....Wataka aachiwe huru
NancyTheDreamtz
Matamshi
ya mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles 'Jaguar' Kanyi kuhusu
kuwatishia raia wa kigeni wakiwemo watanzania wanaofanya kazi nchini
Kenya yaliwasilishwa jana mbele ya kikao cha bunge ili kujadiliwa.
Baadhi ya wabunge nchini humo wakichangia mjadala huo wameunga mkono kauli ya Jaguar huku wakitaka aachiwe huru kwani alichosema ndio mtazamo wa Wakenya waliowengi.
Baadhi ya wabunge nchini humo wakichangia mjadala huo wameunga mkono kauli ya Jaguar huku wakitaka aachiwe huru kwani alichosema ndio mtazamo wa Wakenya waliowengi.
Akichangia
maoni bungeni jana Juni 26, 2019, Mbunge wa Garissa mjini, Aden Duale
amesema Jaguar alifanya jambo la kizalendo kwani Taifa hilo linahitaji
kuwalinda wananchi wao kwenye masuala ya kibiashara.
Mbunge
mwingine ni Moses Kuria wa jimbo la Gatundu Kusini, Amesema kuwa kauli
ya Jaguar sio ngeni kwani viongozi wengi wa nchi hiyo walishawahi
kuongea kuhusu wageni kupora fursa za kibiashara nchini humo.
Jana
Mbunge wa jimbo la Starehe, Jaguar alishikwa na maafisa polisi katika
viunga vya bunge la nchi hiyo na mpaka sasa bado hajaachiwa.
==>.Wasikilize hapo chini
==>.Wasikilize hapo chini
Comments