Wananchi 13,234 Wapatiwa Elimu Ya Madhara Ya Mimba Za Utotoni
NancyTheDreamtz
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Jumla ya wananchi 13,234 wamefikiwa na elimu ya madhara ya mimba za utotoni hapa nchini .
Hayo
yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo
ya jamii,jinsia wazee na watoto Dokta Faustine Ndugulie wakati akijibu
swali la mbunge wa Viti Maalum Fatma Tafiq aliyehoji,ndoa za utotoni
ni tatizo kubwa katika jamii zetu hususan katika jamii zenye umasikini
,je ,serikali haioni kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa umma hasa
katika maeneo ya vijijini ili wananchi wafahamu athari za kuozesha
watoto katika umri mdogo.
Katika
majibu yake,Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na
watoto Dokta Ndugulile amesema serikali ina tambua umuhimu wa elimu kwa
umma katika kupambana na ndoa za utotoni ambazo zina madhara makubwa kwa
watoto wa kike .
Hivyo
amesema kupitia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo TV,Radio,Magazeti na
Majarida serikali imekuwa ikitoa elimu kwa kuandaa jumbe mbalimbali
kuhusu madhara ya mimba za utotoni sambamba na kusisitiza wazazi na
walezi na jamii kwa ujumla kutoozesha watoto Mapema.
Aidha,Dokta
Ndugulile ,amesema, Kwa kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka
,2018,Jumla ya Wananchi 13,234 wamefikiwa na Elimu ya Madhara ya Mimba
za utotoni .
Kati
ya hao,wanafunzi 8,546,walimu 476,viongozi wa dini 110,wazee wa mila
na watu Mashuhuri 90,ngariba 38,waendesha bodaboda 261,wazazi/walezi
3600 na watendaji wa vijiji 113.
Kampeni
ya kutokomeza mimba za utotoni ijulikanayo’mimi Msichana Najitambua
ilizinduliwa mkoani Mara mwaka 2017 ambayo tayari imefanyika katika
mikoa ya Shinyanga,Mara,Tabora,Lindi,Dodoma,Tanga,Dar es Salaam na
Katavi.
Mikoa
6 yenye kiwango kikubwa cha mimba za utotoni hapa nchini Tanzania ni
Shinyanga,Dodoma,Tabora,Mara,Katavi na Singida na takwimu zinaonesha
kuwa asilimia 27% ya mabinti walio chini ya miaka 18 wana mimba au
wamezaa.
Comments