MOSHI: Wananchi wenye hasira kali wachoma moto Kanisa, Wamtuhumu Mchungaji kusababisha vifo vya watoto wawili (+Video)

NancyTheDreamtz
Wanawake waliojawa na jazba wamechoma moto kanisa la Unyakuo lililopo kata ya Msaranga manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa kumtuhumu mchungaji wa Kanisa hilo, kujifanya mkunga jambo ambalo limesababisha vifo vya vichanga wawili ambao walikuwa ni mapacha.
Wakiongea na kituo cha runinga cha Azam TV, Wananchi hao wamesema kuwa Mchungaji huyo alikuwa anawadanganya wanawake wajawazito kuwa wasiende Kliniki, Elimu ambayo imewapotosha watu wengi.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele