Sylvestre Ilunkamba Achaguliwa Waaziri Mkuu mpya DRC

NancyTheDreamtz
Hatua ya Rais Felix Tshisekedi kumteua Profesa Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa waziri mkuu mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imepokelewa kwa hisia mseto.

Uteuzi huo umefanyika baada ya waziri mkuu aliyekuwepo Bruno Tshibala, kujiuzulu.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi wake alisema waziri huyo mkuu alielezea kipaumbele ya serikali yake itakayoundwa baadaye.

''Rais alinipokea na aliniambia ya kwamba kipaumbele cha serikali hii yetu ya muungano ni ni kuboresha maisha ya raia na kurejesha usalama'' alisema Bw. Illunga.

Pia alimshukuru rais wa zamani Joseph Kabila kwa kupendekeza jina lake ali ateuliwe kuwa waziri mkuu.

Raia wa Congo walikua wamesubiri zaidi ya miezi mitatu, bila ya kuwa na waziri mkuu mpya.

Slyvestre Illunga aliwahi kutumika chini ya utawala wa Mobutu Seseko kama mshauri wake wa maswali ya uchumi.

Kutokana na uzoefu wake katika masuala ya uongozi baadhi ya raia wana matumaini kuwa waziri mkuu huyo mpya ataleta mabadiliko hususan katika kupambana na rushwa ambayo imetajwa kuwa tatizo linalorudisha nyuma taifa hilo la maziwa makuu.

''Kulingana na nafasi yake ya kazi tunaamini ataongoza nchi yetu. Tunatumaini experience yake itamsaidia kung'amua wale ambao wataweka mbele maslahi ya nchi na wala sio kubomoa nchi'' alisema mmoja wa wakaazi alyezungumza na BBC.


Mwanasisia huyu mwenye umri wa miaka 78 ambae pia ni miongini mwa viongizi wa chama cha Joseph Kabila, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya reli ya Congo.

Tangu mwaka 2014 waziri mkuu huyu mpya alikuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya reli na wafanyi kazi wengi wa kampuni hiyo wamefanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa mishahara yao.

Wakosoaji wake wanasema hiyo ni dalili mbaya ya kuonesha kwamba hatajibu haraka mahitaji yao.

''Sisi tulikua hatumjui lakini tuliposikia alikua mkurugenzi wa shirika la reli nchini tumeshangaa kwasababu hilo shirika limekufa tayari'' alisema mmoja wao.

Alidai kuwa shirika hilo lilipoteza fedha nyingi nchi ya uongozi wake na mambo mwengine mengi yalifanyika hali ambaye anasema ililemaza huduma zake.

''Sasa wamemfanya kuwa waziri mkuu, je nchi nayo haitakufa?'' aliuliza.

Rais Tshisekedi hata hivyo ameahidi kuwa serikali yake itakabiliana vilivyo na visa vya rushwa.

Kwa mujibu wa vyama vilivyomuunga mkono Joseph Kabila kulingana na jinsi walivyo na idadi kubwa ya waakilishi katika bunge la kitaifa, lile la seneti na majimboni wana haki ya kupewa 80% ya wizara huku wakidai chama cha rais mpya kinafaa kupewa 20%.

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)