Mwanariadha wa kike wa Kenya asema hawezi kupunguza homoni za kiume

NancyTheDreamtz
Bingwa wa mbio za mita 800 nchini Kenya kwa upande wa akina dada Margeret Nyairera Wambui amesema kuwa hatotumia dawa za kupunguza homoni za kiume ili kushiriki katika mbio hizo.

Akihojiwa na BBC mwanariadha huyo amesema kuwa dawa hizo zina kemikali ambazo huenda zikakuathiri katika maisha ya baadaye.

''Mimi siwezi kutumia dawa kwa lengo la kutaka kupata fedha,Mungu aliniumba niwe hivi nilivyo - kumbuka dawa hizi zina kemikali ambazo madhara yake baadaye huenda yakawa mabaya katika mwili wako. Wakati huo wote IAAF haitakuwa hapo''.

Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 24 ni miongoni mwa wanariadha walioathiriwa na sheria mpya ya shirikisho la riadha duniani IAAF inayowataka wanawake walio na viwango vya juu vya homoni za kiume testosterone kutumia dawa ili kuzipunguza mwilini.


IAAF inasisitiza kuwa sheria hiyo ni nzuri katika kuleta usawa katika mashindano , ikihoji kwamba wanariadha wenye homoni za kiume wanafaidika kutokana na ongezeko la nguvu katika mifupa yao na misuli sawa na wanaume walio balehe.

Lakini mwanadada huyo wa Kenya analalamika kwamba tangu Shirikisho la riadha duniani IAAF liidhinishe sheria hiyo maisha yake yamebadilika na kuwa magumu.

''Kwa sasa unajipata umeketi kitandani hujui ufanye nini, ukiamka hujui uende wapi kufanya mazoezi na hata ukifanya mazoezi hujui utakwenda wapi. Hii ndio biashara tunayofanya, ndio inatupatia kila kitu cha kunywa, mahitaji yote, inatusaidia kuwekeza halafu unaamka siku moja unaambiwa sasa kuanzia leo huezi kuendelea na bishara hiyo-lazima maisha yako yataathirika kidogo'', alisema bingwa huyo wa mita 800.

Alitarajiwa kushiriki katika mbio za IAAF World Challenge mjini Nanjing wiki ijayo lakini sasa maisha yake yamegubikwa na swali gumu.

''Usiku usingizi unapotea unajua ni kitu inahusisha maisha yako kwa sababu tayari ulikuwa na malengo yako lakini sasa malengo hayo yamekatizwa'',aliongezea.

Sheria hiyo mpya inaathiri kuanzia mbio za mita 400 hadi maili moja na inashirikisha mbio za Heptathlone zenye vitengo saba ambapo mshindi hukamilisha mbio hizo kwa kushiriki mbio za mita 800.

Nyairera anasema kuwa hawezi kuhamia katika mbio za mita 5000 akisema kwamba hajawahi kushiriki mbio yoyote mbali na ile ya mita 800 ambapo ujuzi na mafunzo tofauti yatahitajika ili kufikia kiwango hicho.

''Sasa kuanza kukimbia mita 5000 kutoka 800 ni kitu hakiwezekani. Sijawahi kukimbia 5000m nikipitia laini ya utepe mara ya kwanza najua kwamba mara ya pili nimemaliza sijawahi kupita Utepe mara hizo zote''.alisema

Chini ya sheria ya IAAF, wanariadha wa kike walio na viwango vya juu vya homoni za kiume watalazimika kushindana na wanaume la sivyo wahamie katika mbio nyengine iwapo hawawezi kutumia dawa kupunguzi viwango vya homoni hizo.

Sheria hiyo mpya itaathiri kuanzia mbio za mita 400 hadoi zile za maili moja na mahitaji yake ni kwamba wanariadha ni sharti wapunguze viwango vyao vya homoni za kiume chini ya kiwango kinachohitajika kwa zaidi ya miezi sita kabla hawajaanza kushindana.

Hatahivyo sheria hiyo mpya imepata wakosoaji huku baraza la haki za binaadamu katika shirika la Umoja wa mataifa likisema kwamba hatua ya kuwaorodheshwa wanariadha wa kike kulingana na viwango vyao vya homoni za kiume inakiuka haki za kibinaadamu.

Hivi majuzi mahakama ya kutatua mizozo katika michezo CAS ilipinga rufaa iliokatwa dhidi ya Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya ambaye ni miongoni mwa wale walioathiriwa na sheria hiyo.

Lakini mahakama hiyo ilisema kuwa ina wasiwasi mkubwa kuhusu matumizi ya sheria hiyo katika siku za baadaye.

Comments

Popular posts from this blog

Mbwana Misosi avurugwa: Unanivimbia wewe nani? mimi staa kabla yako, kama wewe sio shabiki yangu basi demu wako shabiki yangu (Video)