Posts

Showing posts from May, 2019

Ntech ICT Technologies

Image
NancyTheDreamtz .                                                                                                                           This is how we continue  with our project in sourthern Tz

RAIS Magufuli Kushangiliwa kwa Nguvu Afrika Kusini Ina Maana Gani kwa Wapinzani wake??

Image
NancyTheDreamtz Marais wengi wameenda kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini 25 May 2019 , lakini mara baada ya jina la Rais wa Tanzania John Magufuli kutajwa kwamba anaingia uwanjani ,Raia wa Afrika kusini walisimama na kushangilia kwa nguvu sana. Umati mkubwa wa wananchi umelipuka kwa shangwe na chereko wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuaishwa kwa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa leo Jumamosi Mei 25, 2019 Kwa Mtazamo Wa kawaida hii inaashiria Rais Magufuli Kukubalika KITAIFA NA KIMATAIFA, Kwa upande wa upinzani Utaendelea Kubeza na kukejeli Hatua Ambazo anafanya Rais Magufuli ila Kwa upande Wangu wapinzani Kufanya hivyo ni Sahihi kwao kwasababu Hauwezi Kutafuta Serikali kwa kusifia Serikali Iliyopo. Wananchi Wanatakiwa kufahamu Wapinzani wanatekeleza Majukumu Yao,ila Ukweli wanaufahamu na Ukweli siku zote Ha

Kocha wa Sevilla Amvulia Kofia John Bocco, Adai Ana Kiwango Kama cha Drogba

Image
NancyTheDreamtz Mkufunzi wa sevia kutoka laliga ya Spain ameshangazwa na uwezo wa john boco drogba kwa kysema hakudhania Kama Tanzania kuna vipaja namna hii!! Alisema namnukuu "I have never been in east Africa especially Tanzania, I used to know some talented from Africa like drogba and keita but to me that young man with number 22 kit is really magnetic, classical and professional" Reporter: would you ever sign him? Why not' any manager would like to work with "booock'o (Spanish articulation) but i know it is not easy to sign a player from simba which is the richest club in central and east africa Reporter, three players from simba with best performance tonight boco excluded? I think kaaagere, nyoni and mkuude performed well Huyu boco hatari sana tusishangae kesho akalambishwa mkataba na sevia' Kila la kheri boko umri unaruhusu Wewe bado kijana mdogo na haujapunguza umri

Mesii Aweka wazi Hatma yake Barcelona Akumbushia Majonzi na Liverpool “Moja ya Timu Ngumu Niliyokutana Nayo Katika Maisha Yangu ni Liverpool”

Image
NancyTheDreamtz Mchezaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye pia ndio kapteni wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina amefunguka mengi kuhusu hatma yake Barcelona na kuongelea kile ambacho watu wamekuwa wakilalamika sana kuhusu wao kutolewa na Liverpool kwenye michuano ya UEFA kwani ndio timu ambayo ilikuwa inategemewa sana. Lakini pia Lionel Messi anafafanua nani anayelaumu kufungwa na majogoo Liverpool Alisema  “Tunapaswa kuomba msamaha kwa mchezo wa pili huko Liverpool, Ilikuwa mojawapo ya uzoefu mbaya zaidi wa kazi ya Messi, alisema wakati akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari. Alipenda kuiwka wazi kwa mashabiki kwamba watajitahidi kushinda Copa del Rey Jumamosi. Barcelona itacheza dhidi ya Valencia mwishoni mwa wiki katika kuwania kombe la Copa del Rey. Messi aliongeza  “Si kwa sababu ya matokeo, lakini kwa sababu ya jinsi ilivyoonekana kwamba hatukushindana. Ilikuwa moja ya uzoefu mbaya zaidi katika m

Samatta Amejibu Vipi Anaianza Safari ya EPL?

Image
NancyTheDreamtz Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayeichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta amefanikiwa kurudi Tanzania salama akitokea Ubelgiji, Samatta amewasili Tanzania akiwa ametoka kuisadia KRC Genk kutwaa Ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Ubelgiji baada ya miaka nane kupita. Samatta baada ya mafanikio hayo tayari watu wameanza kuuliza kuhusiana na mipango yake ya siku za usoni kama ataendelea kuichezea KRC Genk katika msimu wa 2019/2020 au ndio anaanza safari mpya kwenda Ligi Kuu England kukamilisha ndoto yake ya kupata nafasi ya kuvichezea vilabu vya huko. “Huwezi kujua kinachokuja mbeleni lakini mimi siku zote tulishakuwa tunaenda kwenye mabanda ya mipira watu wengi wanayajua, mimi nilikuwa mmoja wao kwenda kuangalia Ligi Kuu ya Uingereza kitu ambacho kilikuwa kinanivutia sana, napenda kwenda kucheza Ligi Kuu ya Uingereza lakini huwezi jua kila kitu kitakachokuja mbele ila tunahisi kitakachokuja”>>>Samatta

Kocha wa Yanga SC ashikilia mikataba ya wachezaji 14

Image
NancyTheDreamtz Uongozi wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna presha na wachezaji ambao utawafanyia usajili msimu ujao kwani tayari kazi hiyo wamemuachia kocha mkuu, Mwinyi Zahera ambaye anashughulikia mafaili yote ya wachezaji. Yanga mpaka sasa wachezaji wake 16 wa kikosi cha kwanza wanamaliza mikataba yao msimu huu hivyo kinachosubiriwa ni kuwaongezea mkataba wale ambao watakidhi vigezo vya kocha. Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa hawashughuliki na masuala ya usajili kazi hiyo wamemuachia Zahera. "Kuhusu usajili sisi tupo vizuri kwanza tunaanza na wachezaji ambao mikataba yao inamalizika na wameonyesha kazi kubwa na kocha akawakubali hivyo hatma yao ipo mikononi mwa Zahera," amesema Mwakalebela. Wachezaji ambao inaelezwa kwamba mikataba yao inakwisha msimu huu ni pamoja na Ramadhani Kabwili,Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma Makapu, Matheo Anthon

Mahakama yaamuru kura kuhesabiwa upya Malawi

Image
NancyTheDreamtz Mahakama yaamuru kura kuhesabiwa upya Malawi Mahakama nchini Malawi imeiamuru tume ya uchaguzi kutotangaza matokeo ya uchaguzi wa rais wa Mei 21 kufuatia malalamiko ya wizi wa kura yaliyotolewa na upinzani. Katika amri hiyo, Mahakama Kuu ilitaka kusitishwa utangazaji wa matokeo ya kura ya rais na kuelekeza kuhesabiwa upya kwa kura za theluthi ya maeneo yaliyoshiriki uchaguzi. Tume ya uchaguzi nchini humo ilisimamisha kutangaza matokeo hayo baada ya kupokea malalamiko 147 kutoka kwa baadhi ya vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo wa Jumanne iliyopita. Chama kikuu cha upinzani cha Malawi Congress (MCP) kinachoongozwa na Lazarus Chakwera, kiliwasilisha malalamiko mahakamani juu ya kile ilichodai kuwa makosa yaliyojitokeza katika wilaya 10 kati ya 28 nchini humo. Ujumbe wa Waangalizi wa Umoja wa Ulaya uliueleza uchaguzi huo kuwa ulisimamiwa vizuri, ulikuwa na uwazi pamoja na ushindani mkali.

Kocha wa Simba SC asaini mkataba mpya

Image
NancyTheDreamtz Koch a wa Simba SC, Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.  Uamuzi wa kumuongezea mkataba umeafikiwa na Bodi ya Wakurugenzi baada ya Kocha Aussems kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

COMPUTER/CCTV /NETWORKING 2019

Image
NancyTheDreamtz Find us for any work in CCTV,COMPUTERS and NETWORKING +255692210119 or +255673050373  

Muna Love "Kazi Yangu Inayoniweka Mjini ni Kufagia Makaburi ya Kinondoni

Image
NancyTheDreamtz MSANII wa filamu ambaye kwa sasa amejikita kwenye muziki wa Injili, Rose Alphonce ‘Muna Love’ amemtolea povu si la nchi hii shabiki wake aliyetaka kujua wapi anapopata fedha za kutanua. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muna alimjibu shabiki anayejiita Anitha_sanga_e ambaye alipoona picha ya Muna mtandaoni humo iliyoonesha anakula bata, ndipo alipomuuliza: “Muna unafanya kazi gani?”  Unataka kujua alijibu nini? Mambo ni moto, hili ndilo lilikuwa jibu lake: “Nafagia makaburi ya Kinondoni mpenzi.”

Nyota Yako Leo Jumanne 21 May 2019

Image
NancyTheDreamtz 🔯NG'OMBE -  (April 21– May 21) Leo hii ukimuona mtu ana ndevu nyeupe, basi ujue hiyo ni ishara ya kuwa mambo yako sasa yatafunguka na kukunyookea, ile mikwamo ya hapa na pale itafunguka kwa urahisi. 🔯MAPACHA - (May 22- Juni 21) Leo katika matembezi yako ukikutana na mwanamme amevaa mkufu wa shanga, hiyo ni dalili ya kupata kila kitu utakachokihitaji bila ya kutumi67a muda au nguvu nyingi.Unashauriwa kuwa mtu wa ibada na kutoa sadaka. 🔯KAA - (Juni 23- Julai 22) Leo Mchana ukikutana na Mwanamme akiwa amevaa Mkufu wa Fedha, hiyo ni dalili ya kutimia kwa ndoto yako ya kupata Mwanamke au Mwanamme mzuri na kutimia kwa Ndoa yako. 🔯SIMBA LEO -  (Julai 24- Agosti 23) Ukimwona mtoto Leo hii analia, basi hiyo ni ishara ya wewe kupata mtoto mzuri au utapata mpenzi mpya ambaye utakutana naye bila ya kutegemea. Sherehe utakayohudhuria itakutanisha na wangu wengi ambao hukutegemea. 🔯MASHUKE - (Agosti 24- Septemba 23) Elewa kuwa ile posa yako imekataliwa na mpenzi unayemt

Mwanamuziki Rihanna Aamua kuja na Albamu ya Reggae

Image
NancyTheDreamtz Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Rihanna anaanda Albamu ya Reggae, Mwaka jana pia alidokeza lakini akapiga tena kimya. Kupitia mahojiano yake mapya na jarida la ‘NY Times’ Rihanna amethibitisha kuwa anaandaa Albamu ya Reggae, Pia amefunguka kuwa bado hajajua jina la Albamu japo mashabiki wengi wanataka iitwe “R9” kwasababu ni Albamu yake ya 9. Pia alipoulizwa kama ana mpango wowote wa kufanya kazi na Drake alisema sio siku yoyote ya hivi karibuni.

Humphrey Polepole apata uteuzi serikalini

Image
NancyTheDreamtz Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama wa Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, ameteuliwa na waziri wa Ardhi William Lukuvi, kuwa mjumbe wa shirika la nyumba la taifa (NHC). Waziri Lukuvi ameteua wajumbe hao 7 wa bodi ya shirika la nyumba la taifa, leo Mei 20, 2019 siku chache baada ya Rais Magufuli kumteua Dr. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo. Wajumbe walioteuliwa ni, 1. Bi. Immaculate Senye 2. Bi. Sauda Msemu 3. Bw. Abdallah Mwinyimvua 4. Bw. Humphrey Polepole 5. Bw. Martine Madeke 6. Eng. Mwita Rubirya 7. Bw. Charles Singili

Mwanariadha wa kike wa Kenya asema hawezi kupunguza homoni za kiume

Image
NancyTheDreamtz Bingwa wa mbio za mita 800 nchini Kenya kwa upande wa akina dada Margeret Nyairera Wambui amesema kuwa hatotumia dawa za kupunguza homoni za kiume ili kushiriki katika mbio hizo. Akihojiwa na BBC mwanariadha huyo amesema kuwa dawa hizo zina kemikali ambazo huenda zikakuathiri katika maisha ya baadaye. ''Mimi siwezi kutumia dawa kwa lengo la kutaka kupata fedha,Mungu aliniumba niwe hivi nilivyo - kumbuka dawa hizi zina kemikali ambazo madhara yake baadaye huenda yakawa mabaya katika mwili wako. Wakati huo wote IAAF haitakuwa hapo''. Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 24 ni miongoni mwa wanariadha walioathiriwa na sheria mpya ya shirikisho la riadha duniani IAAF inayowataka wanawake walio na viwango vya juu vya homoni za kiume testosterone kutumia dawa ili kuzipunguza mwilini. IAAF inasisitiza kuwa sheria hiyo ni nzuri katika kuleta usawa katika mashindano , ikihoji kwamba wanariadha wenye homoni za kiume wanafaidika kutokana na ongezeko la nguvu kati

Sylvestre Ilunkamba Achaguliwa Waaziri Mkuu mpya DRC

Image
NancyTheDreamtz Hatua ya Rais Felix Tshisekedi kumteua Profesa Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa waziri mkuu mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo imepokelewa kwa hisia mseto. Uteuzi huo umefanyika baada ya waziri mkuu aliyekuwepo Bruno Tshibala, kujiuzulu. Akizungumza na vyombo vya habari baada ya uteuzi wake alisema waziri huyo mkuu alielezea kipaumbele ya serikali yake itakayoundwa baadaye. ''Rais alinipokea na aliniambia ya kwamba kipaumbele cha serikali hii yetu ya muungano ni ni kuboresha maisha ya raia na kurejesha usalama'' alisema Bw. Illunga. Pia alimshukuru rais wa zamani Joseph Kabila kwa kupendekeza jina lake ali ateuliwe kuwa waziri mkuu. Raia wa Congo walikua wamesubiri zaidi ya miezi mitatu, bila ya kuwa na waziri mkuu mpya. Slyvestre Illunga aliwahi kutumika chini ya utawala wa Mobutu Seseko kama mshauri wake wa maswali ya uchumi. Kutokana na uzoefu wake katika masuala ya uongozi baadhi ya raia wana matumaini kuwa waziri mkuu huyo mpya ataleta m

Mbunge wa CCM Aitaka Serikali Kuhusu Kilimo cha Bangi Bangi Tanzania

Image
NancyTheDreamtz Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ameishauri Serikali ya Tanzania kuruhusu kilimo cha bangi nchini kwa ajili ya utengenezaji wa dawa za binadamu. Amesema hayo leo Jumatatu Mei 20, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020. Amesema nchi nne Barani Afrika zimeruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa za binadamu. “Amebainisha dawa nyingi za maumivu ya saratani asilimia 80 zinatokana na bangi, “Nashangaa wataalam wetu wa Mamlaka ya Chakula la Dawa (TFDA) wangekuwa wameshachukua sampuli na wangewajulisha kuwa dawa zilizo na bangi ndani yake.” “Wangemuuliza msambazaji hiyo bangi anaitoa wapi? Spika sisi wenyewe tunayo bangi hiyo tunaona kila siku inakatwa ukweli nyingi sio kwa ajili ya kuvuta. Bangi hiyo imekuwa ikienda katika dawa za binadamu.” Amesema ana ushahidi Lesotho na Zimbabwe kuruhusu ulimaji wa bangi na kuna viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu kwa kutumia bangi. Amesema gunia moja la b