Kocha wa Yanga SC ashikilia mikataba ya wachezaji 14

NancyTheDreamtz

Uongozi wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna presha na wachezaji ambao utawafanyia usajili msimu ujao kwani tayari kazi hiyo wamemuachia kocha mkuu, Mwinyi Zahera ambaye anashughulikia mafaili yote ya wachezaji.

Yanga mpaka sasa wachezaji wake 16 wa kikosi cha kwanza wanamaliza mikataba yao msimu huu hivyo kinachosubiriwa ni kuwaongezea mkataba wale ambao watakidhi vigezo vya kocha.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa kwa sasa hawashughuliki na masuala ya usajili kazi hiyo wamemuachia Zahera.

"Kuhusu usajili sisi tupo vizuri kwanza tunaanza na wachezaji ambao mikataba yao inamalizika na wameonyesha kazi kubwa na kocha akawakubali hivyo hatma yao ipo mikononi mwa Zahera," amesema Mwakalebela.

Wachezaji ambao inaelezwa kwamba mikataba yao inakwisha msimu huu ni pamoja na Ramadhani Kabwili,Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Said Juma Makapu, Matheo Anthony, Thabani Kamusoko, Raphael Daudi, Pius Buswita, Juma Mahadhi, Baruani Akilimali, Amissi Tambwe, Haruna Moshi.

Comments

Popular posts from this blog

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele

Top Ten ya Makabila Yaliyotoa Wasomi Wengi Nchini Tanzania

Jacqueline Wolper Atamani Kutoka Kimapenzi na Rais