Wapinzani DRC Watishia kuandamana kupinga mfumo wa upigaji kura

NancyTheDreamtz
Wapinzani DRC Watishia kuandamana kupinga mfumo  wa upigaji kura
Wagombea wakuu wa upinzani kwa nafasi ya urais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, upinzani umeitisha maandamano ya kupinga mfumo wa kura kwa mashine za elekroniki kwenye uchaguzi mkuu wa Desemba 23. Upinzani unasema kuwa wanapinga pia daftari la wapigakura wasio na alama za vidole kwenye kadi zao. Hata hivyo, Martin Fayulu, mmoja wa wagombea wa urais na ambaye alisoma taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani mbele ya waandishi wa habari mjini Kinshasa, alisema upinzani hauna nia ya kuususia uchaguzi huo.



“Tunawatolea wito raia wa Kongo kujipanga kwa ajili ya kulazimisha kuweko na kura ya makaratasi kulingana na sheria ya uchaguzi na kalenda iliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi.”

Licha ya hayo, wapinzani walisema wanaunga mkono juhudi zozote za mazungumzo ili kupata suluhisho kuhusu mfumo wa uchaguzi wa matumizi ya mashine ya elekroniki.

Taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani iliidhinishwa na Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Jean-Pierre Bemba, Moise Katumbi, Freddy Matungulu na Martin Martin Fayulu.

Hatua hiyo ya upinzani ilikuja siku moja baada ya kuvunjika kwa mkutano wa pili na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) kujadili changamoto za kiufundi katika maandalizi ya uchaguzi. Mwenyekiti wa tume hiyo, Corneille Nangaa, alisema kwamba upinzani ulikwenda na ajenda na masharti yake.



Jean-Pierre Bemba, kiongozi wa upinzani aliyezuiwa kuwania urais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakati huo huo, katika kuunga mkono mkutano wa hadhara wa upinzani wa Jumamosi (13 Oktoba) mjini Lubumbashi, gavana wa zamani wa Katanga, Moise Katumbi, alisema kupitia ujumbe wa vidio kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba CENI haikuwa imeweka mazingira ya uchaguzi huru.


Martin Fayulu, président de l’ECIDE, le 23/03/2017 à Kinshasa. Radio Okapi/Ph. John Bompengo
Kauli yake ilikuwa siku moja baada ya kesi yake iliyofunguliwa wiki hii kuhusu mashtaka ya kuajiri mammluki kwa madhumuni ya kuipindua serikali ya Rais Joseph Kabila kuahirishwa baada ya jaji kwenye Mahakama ya Katiba kusema haiwezi kufunguliwa pasina kuwepo kwa mshukiwa binafsi.

Katumbi amekataliwa ruhusa kurudi nchini Kongo kutoka uhamishoni.

Comments

Popular posts from this blog

UCHAGUZI KENYA: Mchezaji wa zamani wa Inter Milan, McDonald Mariga kutoana jasho na Prezzo

Siri Yafichuka, Prince Dube Anakwenda Yanga Kuziba Nafasi ya Fiston Mayele